Thursday, April 28, 2011

early Pregnancies in Tanzania (Talking notes on a TV Talk show)

Balaa au baraka kuzaliwa msichana Tanzania?

Ninajiuliza sipati jibu kama kweli Serikari na jamii ya kitanzania imeshindwa kutowesha tatizo la mimba za wanafunzi. Takwimu zinatisha!

Ukubwa wa tatizo
• Takwimu za wizara: kutokana na mimba kila mwaka wasichana 8,000 hawamalizi shule, ambapo 5,000 ni shule za misingi na 3,000 ni sekondari.

BEST(Basic Education Statistics of Tanzania) - 2004- 2008: Wasichana 28,590 hawakumaliza ambapo 11,599 ni wa sekondari na 16,991 wa shule za misingi

BEST 2009: Wasichana 6345 (waliogundulika tu na kuthibitishwa) hawakumaliza sekondari kutokana na mimba na 11,264 kutokana na utoro (mimba na ndoa za utotoni zikiwemo)

Takwimu zaidi (school girl pregnancies, national situation causes and impact ya MOEVT: 2004- 2009) wasichana 36,705 walipata ujauzito

Tatizo linakua kila mwaka. Mf. Mwaka 2004 zilitibishwa mimba 772 ikaongezeka kuwa 4,965 mwaka 2008 kutoka shule za sekondari pekee

• Lindi pekee: kila mwezi wasichana 5 hupata mimba (The citizen Julai 2010)

• Tanga 2009: wasichana 300 (Nipashe Machi 15,2010)

• Kagera 2009: wasichana 880(Jambo leo January 12, 2010)

• asilimia zaidi ya 15 ya watoto wote walioacha shule mwaka 2009 ilisababishwa na mimba za utotoni.

Vyanzo
• Ubakaji (Mf. Karagwe angalau watoto 54 walibakwa mwaka 2009)
• Wanafunzi kupanga mitaani (Gheto) (Mf. Singida kuna sec schools 153 ila zenye mabweni ni 21 tu)
• Mila potofu (jando, unyago, kutoa wari)
• Umaskini wa wazazi
• Umbali na usafiri wa shule
• Ujinga na nguvu kidogo ya kushinda vishawishi
• Elimu duni juu ya afya ya uzazi
• Kutoshughughulikiwa na duty bearers (Madiwani, wabunge, n.k)

Madhara ya mimba za utotoni
• Kufa kwa ndoto zao watoto
• Kupoteza uhai kutokana na utoaji mimba
• Maambukizo ya VVU (Mf. Karagwe mwaka 2008 asilimia 85 ya waliopata ujauzito ambao ni 102 walipata maambukizo)
• Maradhi yatokanayo na uzazi mf. fistula
• Kudharaulika kwa elimu ya mtoto wa kike
• Umaskini endelevu ktk jamii
• Uadui ktk jamii

Ugumu wa kesi
• Mianya ya rushwa
• Kuyamaliza kifamilia
• Udanganyifu wa wahusika
• Vitisho kwa wasichana
• Kukosa ujasiri wa kujitetea
• Umbali kufikia dola
• Muda mrefu wa kesi na gharama (mf. Karagwe kesi 167 mwaka 2008 ni kesi 12 zilizoshughulikiwa hadi 2010)

Nini kifanyike
• Ujenzi wa mabweni kwa shule zisizo na mabweni, ulinzi na elimu ya umuhimu wa mabweni
• Mafunzo kwa walimu wa afya na malezi
• Semina za mara kwa mara za kujitambua kwa vijana na upimaji wa mara kwa mara: mashuleni, maeneo ya ibada, n.k
• Kamati za shule, Madiwani na wabunge kuwajibika
• Vyombo vya dola kusimamia kesi ipasavyo
• Chakula cha mchana shule za kutwa
• Tuwaache watoto wawe watoto
• Utekelezaji wa re-entry policy

Sera ya Re entry
• Kwanza tukazanie kupunguza tatizo
• Watoto wasamehewe. Makosa yao yana misingi ambayo wazazi na jamii kwa ujumla wamechangia
• Wapewe fursa ya kuwa watoto tena na wajifunze kutokana na makosa yao (walimu wa malezi, washauri na wanasaikolojia)
• Wasaidiwe ulezi wa watoto wao
• Waandaliwe utaratibu wa kuhudhuria masomo/mitihani yao bila unyanyapaa.(ref. Nganza, au madarasa ya jioni)
• Wale wote wanaowapatia wanafunzi mimba wanawajibishwa kisheria pamoja na kulazimishwa kulipia gharama yote ya kukatisha masomo na malezi ya mtoto hadi mtoto afikapo miaka 18. Na wale ambao wanafanya vitendo hivyo kwa mabinti wa chini ya miaka 18 washtakiwe kwa mujibu wa sheria kwa makosa ya ubakaji (statutory rape).
NB:
Tanzania imepoteza mabinti wengi walioachishwa shule kwa sababu ya ujauzito ambao kama wangepata nafasi ya kuendelea na shule wangeweza kutoa mchango kwa taifa

Article 26 of the Universal Declaration of Human Rights says: “Everyone has the right to education…education shall be directed to the full development of the human personality.” That access to education for girls needs to be granted and protected to making sure that they acquire full development of their personalities